Ebola
Mambo ya kujuwa kuhusu ugonjwa wa Ebola
Ebola ni nini ?
Ebola ni ugonjwa mbaya ambao unasababisha kifo kama hautunzwe haraka. Ugonjwa huo umepewa jina hilo la mto uitwao Ebola wenye kuwa katika sehemu ya kaskazini mwa jamhuri ya kidemocrasia ya Congo (RDC), ambako ugonjwa huo umejitokeza kwa mara ya kwanza munamo mwaka wa elfu moja mia tisa makumi saba na sita, 1976.
Ginsi mtu anagonjwa ?
Ugonjwa wa Ebola unajitokeza mtu akiisha kugusa damu ao mikojo, mavi, mate, vitapikiyo, maziwa ya mwanamke, jasho, maji ya uzazi ao vitu vingine vilivyo ambukizwa na mgonjwa wa Ebola. Ugonjwa wa Ebola unaambukiya pia kiisha kukutana na nyama za bora zenye kugonjwa ao zilizo kufa.
Utaratibu gani wa kuchukuwa ?
Mtu anaweza kujikinga akichukuwa mipango ya utaratibu ifwatayo : kunawa mikono, kuepuka kukutana na mikojo, mavi, mate, vitapikiyo, maziwa ya mwanamke, jasho, maji ya uzazi, vyote hivi vikiwa vimehakikishwa kuwa na Ebola. Jambo lingine ni kuacha kugusa maiti ya mifu.
Je, kuna chanjo ya kuponya Ebola ?
Ndio, maelfu ya watu wamepewa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola katika magonjwa ya gonjwa yaliyopita. Ugavi wa kimataifa wa kipimo cha chanjo umeundwa na UNICEF, WHO, IFRC na MSF kujibu haraka magonjwa ya milipuko ya baadaye.
Vitambulisho ni gani ?
Vitambulisho vinapishana. Mwanzoni, vitambulisho kamilifu ni sawa vile homa kali ya kifudifudi,uzaifu mkali wa mwili, maumivu ya viungo vya mwili, maumivu ya kichwa na shingo. Vivyo hivyo, mgonjwa anatapika na kuhara. Kwenye mwili wake kunaota vidonda. Kiisha hapo kunajitokeza maumivu ya figo. Mwishowe, mwili wote unavuya damu ndani na njee.
Wakati gani ugonjwa unajitambulisha ?
Mda wa kujisimika katika mwili unaanza tangu ugonjwa umeambukizwa siku mbili ao siku makumi mawili na moja. Wakati huo, mgonjwa haweze kuambukiza kabla vitambulisho havionekane. Ni matokeyo ya vipimo ndiyo inaweza kuhakikisha ugonjwa wa Ebola.
Tufanye-je ugonjwa unapojionyesha vitambulisho ?
Unaposhikwa na homa kali kiisha kukutana na mgonjwa wa Ebola ao kiisha kushiriki kwenye mazishi, enda haraka kwenye chumba cha matunzo chenye kuwa karibu. Huko, utapimwa ginsi ilivyo na kuarifiwa ginsi ya kukinga jamaa lako nzima na majirani wengine.
Yawezekana kutunza Ebola nyumbani ?
Hapana ! Watu wenye kuwa na vitambulisho vya ugonjwa wa Ebola wanalazimishwa kujielekeza hima kwenye hospitali ao chumba cha matunzo munamo kuwa waganga na wa-uguzi wenye kuwa na vyombo kamilifu vya kutunza ugonjwa huo.
Je, yawezekana kupona ao là ?
Mtu yeyote mwenye kuwa mgonjwa wa Ebola anaamurishwa ajitambulishe kwa haraka ginsi ilivyo. Madawa mawili zimeongeza idadi ya uponyaji wa wagonjwa zinapotumiwa kwa haraka.
Kuna nini kiisha hapo ?
Inafahamishwa kuwa, watu waliokwisha kupona hawaweze tena kuambukiza wengine . Hata hivyo, ugonjwa wa Ebola unabaki katika maji ya uzazi mda wa myezi mitatu. Ndiyo maana, waliopona wanaombwa kuvaa mupira mda wa kitendo cha ndowa.